YANGA YASHINDWA KUVUNJA REKODI HII

Kikosi cha Yanga chenye mabadiliko makubwa msimu huu kimeshindwa kuivunja rekodi yake ya msimu uliopita ya 2018/19 kwa kuipoteza kabisa rekodi yao ya msimu uliopita.


Rekodi zinaonyesha kwamba msimu wa 2018/19 Yanga ikiwa na staa mkubwa Heritier Makambo pekee kwenye mechi nne sawa na dakika 360 walivuna jumla ya point 12 na walikuwa vinara wa ligi kwani hawakupoteza mchezo hata mmoja.

Yanga iliyokuwa inaongozwa na Kelvin Yondan akiwa ni nahodha mkuu kabla ya kupigwa chini ilishinda mbele ya Mtibwa Sugar mabao 2-1 ikaipiga Stand United mabao 4-3 kabla ya kuikandamiza Coastal Union bao 1-0 na ikashushia pumzi  kwa Singida United kwa mabao 2-0.

Kwenye mechi nne Yanga ilifunga jumla ya mabao 9 na ilikubali kufungwa mabao manne pekee huku beki wa kwanza kufunga bao kwa msimu huo ndani ya Yanga akiwa ni Kelvin Yondan aliyefunga dakika ya 40 kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kwa penalti na mechi zote zilichezwa uwanja wa Taifa.

Mambo yamekuwa tofauti msimu huu ambapo Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ina mastaa wa kutosha ikiwa ni pamoja na David Molinga mtaalamu wa kupiga mipira iliyokufa pamoja na beki mwili jumba Lamine Moro imeambulia jumla ya pointi 7 ikizipoteza pointi 4.

Imefunga jumla ya mabao sita na imefungwa mabao manne ndani ya dakika 360, mchezo wake wa kwanza ilifungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting uwanja wa Uhuru kabla ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na Polisi Tanzania na ilishinda mbele ya Coastal Union bao 1-0 na mbele ya Mbao FC bao 1-0.

Zahera amesema kuwa mabadiliko makubwa ndani ya kikosi yanaifanya timu yake kushindwa kupata matokeo kutokana na kukosa muunganiko mzuri

Post a Comment

0 Comments