KIKOSI CHA YANGA CHAONDOKA KUELEKEA MISRI JIONI HII

Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 8 kimeondoka jioni ya leo tarehe 31/10/2019 kuelekea nchini Misri kwa mchezo wa marudiano.


 Yanga watafika jijin Cairo na moja kwa moja wataanza mazoezi yamwisho kuwakabili Pyramids siku ya jumapili tarehe 3/11/2019 kwenye dimba la 30 June. Mchezo huo utakuwa wa mkali sana kwani Yanga wamejiandaa vyema na hawata taka kufanya makosa waliyoyafanya mchezo wa kwanza uliopigwa CCM Kirumba jijini mwanza na Yanga kufungwa mabao 2-1.

Yanga italazimika kucheza kwa tahadhari kuwazuia Pyramids wasipate goli na watatakiwa kushambulia zaidi ili wapate magoli 2-0 au 3-1 ili waweze kufuzu hatua ya makundi.

Sare yoyote itaifanya Yanga itoke kwenye michuano hiyo. Mwalimu zahera anaonekana kuja na mbinu mbadala za kuwadhibiti Pyramids. 

Uongozi wa klabu hiyo umesema wachezaji wote waliokwenda misri wako fiti na hakuna yeyote mwenye majeraha  na kusisitiza ushindi kwenye mechi hiyo.


Post a Comment

0 Comments