JE ARSENAL NA CHELSEA ZITAWEZA KULIPA KISASI KWA LIVERPOOL NA MANCHESTER UNITED?

Klabu ya Arsenal inakibarua kigumu kuhakikisha inalipa kisasi kwa Liverpool. Timu hizo zinakutana kwa mara ya pili baada ya mchezo wa kwanza wa  Ligi Kuu uliomaliza kwa Liverpool kushinda 3-1


Liverpool itaikaribisha tena Arsenal kwenye mchezo wa kombe la Carabao. Mchezo huo utachezwa saa 10;30 usiku na atakayefungwa basi atakuwa ameyaaga mashindano hayo.

Liverpool imekuwa kwenye kiwango kizuri zaidi msimu huu baada ya kucheza michezo 10 na kutoa sare mchezo mmoja tu dhidi ya Manchester United  huku michezo 9 ikishinda na kujikusanyia pionti 28. .

Arsenal naye anasogea vizuri kwani amecheza mechi 10 za ligi akishinda mechi 4 sare 4 na kufungwa 2, klabu hiyo inapointi 16 na inashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi.

Mchezo mwingine ni kati ya Manchester United  vs Chelsea utakaopigwa kuanzia 11:00 usiku . mchezo wa kwanza ligi kuu msimu huu Manchester United waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wababe hao wa London.  Mchezo huo utapigwa dimba la Stamford Bridge.


Chelsea imerejea kwenye fomu ya uchezaji ikiwa imecheza michezo 10 ikishinda michezo  6 ikitoka sare 2 na kufungwa 2. klabu hiyo imejikusanyia pointi pointi 20 na ipo nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza. Mchezo wa mwisho kwenye ligi ilicheza na Burnley na ilishinda mabao 4-2.

Manchester United wameanza kurejesha makali mara baada ya kuanza vibaya msimu huu . klabu hiyo imecheza mechi 10 imeshinda 3 sare 4 na kufungwa 3 ikijikusanyia pointi 13 na kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 7.

Timu hizo zinatakiwa kushinda mechi zao ili ziweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Kombe la Ligi (EFL-CARABAO).

Post a Comment

0 Comments