HATIMAYE LIPULI YAISHTAKI POLISI TANZANIA KWA TFF


Lipuli imelaani kitendo cha jeshi la polisi mkoani iringa kuwapiga na kuwakamata wachezaji wa klabu hiyo pasipo makosa kuwekwa wazi usiku wa jana Oktoba 30, 2019, 


Leo viongozi wa Klabu hiyo wameliomba shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuingilia kati vitendo hivyo ili kuendeleza mpira wa Tanzania.

Katika muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Lipuli  yenye maskani yake mkoani Iringa imewaalika polisi Tanzania kutoka mkoani Arusha , lakini jana majira ya saa tatu usiku baadhi ya wachezaji wa lipuli akiwamo nahodha Paul Nonga, walikamatwa na polisi bila sababu za msingi.
Mwenyekiti wa Lipuli FC anasema kutokana na fujo za hapa na pale, imesababisha wachezaji kuumia na kutolewa nje ya mchezo kisaikolojia huku Issa Rashid akilazimika kupelekwa hospitali kutokana na maumivu makali aliyoyapata.
Katibu wa chama cha soka Iringa Ally Ngala ameeleza.
Sisi kama Amo Media Group tunalaani vikali kitendo hicho cha jeshi la polisi kwa kufanya mambo yasiyofaa kwenye jamii na tunaomba maaskari husika wachukuliwe hatua kali za kisheria kwani hiyo ni dalili ya rushwa.

Post a Comment

0 Comments