BONDIA HASSAN MWAKINYO ATANGAZA KUMPIGA MFILIPINO ,ALAMBA DILI NONO ZAIDI

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amelamba dili nono kuelekea mpambano wake na bondia kutoka Ufilipino Arnel Tinampey atakayepambana naye Novemba 29 mwaka huu


Pambano hilo litafanyika uwanja wa taifa na mashabiki wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono bondia huyo aliyecheza mapambano 17 akishinda mapambano 15 na kupigwa mapambano 2 tu huku pia akiwapiga wappinani wake kwa Knock Out (KO) 11. 

Mwanyiko ni bondia namba 1 Africa kwa ubora uzito wa .....na duniani anashika nafasi ya 19 na unapotaja mabondia 50 bora  duniani basi Mwakinyo ni bondia  pekee kutoka Afrika katika orodha hiyo.
Mwakinyo amesema mpinzani wake raia wa ufilipino hajawahi kupigwa hivyo ajiandae kupigwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania. 
Mwakinyo ametoa kauli hiyo mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kurusha pambano hilo kati ya Kituo  cha televisheni kitakachorusha mpambano huo  na Kampuni ya Hall of Fame kupitia kwa promota wake Jay Msangi

Post a Comment

0 Comments