Klabu ya Simba hapo jana ilifungwa bao 1-0 na Mwadui FC ya mkoani Shinyanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Huo ni mchezo wa kwanza kwa Simba kufungwa
Msimu huu.na klabu hiyo ilikuwa imecheza michezo 6 na ilishinda yote hivyo kuwa kileleni mwa ligi kwa pointi 18.
Mara baada ya mechi kukamilika nahodha wa Mwadui FC Joram Mgeveke alifanya mahojiano na mtangazaji wetu kuhusiana na matokeo hayo na alisema " Ni kujituma kwetu na kufuata maelekezo ya mwalimu"
Michezo mingine ya ligi kuu Tanzania itaendele leo na kuzikutanisha klabu za Alliance vs Mbeya City mchezo utakaopigwa uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
0 Comments