Klabu za Arsenal na Liverpool usiku wa kuamkia leo zimeishangaza dunia baada ya kutoka sare ya mabao 5-5. Mchezo huo wa Kombe la ligi maarufu kama Carabao Cup ulipigwa
Katika dimba la Anfield na hakuna shabiki alietegemea kuona matokeo hayo ya ajabu,Timu hizo zilitumia wachezaji wengi chipukizi na mpaka dakika ya 90 matokeo yalikuwa Arsenal 5 na Liverpool 5.
KIKOSI cha Liverpool kimesonga hatua ya Robo Fainali ya Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 5-4.
Sare ya mabao 5-5 ilipelekea timu hizo kupigiana penalti ambapo Arsenal ilishinda penalti 4 na kukosa moja huku Lierpool ikishinda penalti zote tano.
Wapigaji kwa upande wa Arsenal ni Bellerin, Guenduozi, Martinell hawa walipata, Ceballos alikosa, Maitland- Niles alipata.
Kwa upande wa Liverpool alianza Milner, Lallana,Brewster Origi na Jones alimaliza kwa kufunga penalti ya ushindi.
0 Comments