ALIYEWAFUNGA YANGA MABAO 3 AMTISHIA NYAU MEDDIE KAGERE

Mshambuliaji wa klabu ya Polisi Tanzania na timu ya Tanzania "Taifa Stars"  ameanza kumtisha mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere  kuwania kiatu cha dhahabu ligi kuu Vodacom.


Ditram Nchimbi alijipatia umaarufu mara baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa uhuru na timu hizo kufungana mabao 3-3.

Mabao 3 ya Nchimbi yanamfanya aingie kwenye kinyang'anyiro cha ufungaji bora  akiwa nyuma ya Miraji Athuman mwenye mabao 4 na Meddie Kagere mwenye mabao 7. Nchimbi anaamini kuwa mchezaji bora si lazima acheze Simba au Yanga na amenukuliwa akisema :

"Naweza kuwa mfungaji bora hata kama nacheza Polisi Tanzania ,kikubwa nachokiomba ni kutopata majeraha nikiwa fiti sidhani kama linashindikana hilo ingawa wapo washambuliaji wengi na wakali. Hayo ni malengo binafsi ila cha muhimu ni kuhakikisha naisaidia timu yangu kuhakikisha inamaliza nafasi nne za juu"

Hapo baadae Nchimbi ataiongoza Polisi Tanzania dhidi ya Lipuli mchezo utakaopigwa dimba la Samora mkoani Iringa ,Huku Simba ikiongozwa na Kagere itakaribishwa na Mwadui mkoni Shinyanga.

Nchimbi hajafunga bao lolote kwenye mechi mbili alizocheza hivi karibuni dhidi ya Singida United na Mwadui. Huku akiisaidia Taifa stars kufuzu michuano ya  CHAN 2020

Post a Comment

0 Comments