ALIKIBA AMJIBU DIAMOND KUHUSU KUSHIRIKI TAMASHA LAKE LA WASAFI FESTIVAL

Huku vuguvugu la Wasafi Festival 2019 likiendelea na kuhamia Dar Es Salaam ambapo Mkurugenzi mkuu wa WCB na mwanamuziki Diamond Platnumz amesema tamasha hilo 

litakuwa la kipekee kuwahi kufanyika Dar Es Salaam amewaalika baadhi ya wasanii akiwemo Ally Kiba na Harminize lakini Ally kiba ameamua kumjibu Diamond.
Ally Kiba amesema kuwa hataki mazoea kama ya wanafunzi wa shule ya msingi na kuonyesha kuwa hataki kabisa kuhudhuria tamasha hilo la Diamond litakalofanyika Jijini Dar es salaam viwanja vya Posta
“Usiniletee mambo ya darasa la pili unaniibia penseli alafu unanisaidia kutafuta. (UNIKOME), Mwanaume huwa anaongea mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema @diamondplatnumz #Kingkiba”
Leo Diamond akiwa katika mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam na litaanza saa 1:00 asubuhi siku ya Jumamosi Novemba 9, 2019 na litamalizika saa 6:00 usiku na kupendekeza msanii huyo Ally Kiba kuwepo sikuhiyo.
Tamasha la Wasafi Festival 2019, tayari limeshafanyika takribani mikoa 7 Tanzania bara ikiwemo Iringa, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga na Dodoma.

Post a Comment

0 Comments