ads

adds

AIBU HII...KWELI SIMBA NA YANGA JIFUNZENI KWA KMC?


KMC au Kinondoni Municipal Council ni timu iliyoanzishwa mwaka 2015 na mwaka 2018 ilipanda ligi kuu na kufanikiwa kumaliza nafasi ya nne msimu wa 2018/19

msimu wa 2019/20 timu hiyo ilifanikiwa kucheza kombe la shirikisho Caf na kuishia raundi ya kwanza , Hayo ni mafanikio makubwa kwa timu ndogo kama hiyo.
Waziri wa 
 habari utamaduni sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe Jumatano ya October 2 2019 alitembelea makao makuu ya club ya KMC yaliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara hiyo waziri Mwakyembe alioneshwa ramani ya ujenzi wa uwanja wa KMC.
Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta ambaye ndio alikuwa mwenyeji wa waziri Mwakyembe alimuonesha ramani ya ujenzi wa uwanja wao mpya utakaojengwa maeneo ya Mwenge na utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 3000.
Baada ya kuona hayo na kusikia mpango wa muda mrefu wa club hiyo ni kujenga academy, waziri Mwakyembe alitoa baraka zake na kuwapongeza kwa hatua hiyo waliyofikia “Kwa uongozi wa malengo na uongozi wa pamoja ambao umefanikisha vitu vingi sana vya mfano kwa wengine”
Simba na Yanga ni vilabu vikongwe ila mpaka sasa havina hata viwanja vya mazoezi. 

Post a Comment

0 Comments