ads

adds

YANGA YASHINDWA KUTAMBA TAIFA DHIDI YA ZESCO UNITED

Klabu ya Yanga imeshindwa kutamba jijini Dar es salaam baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zesco. Yanga walianza mchezo huo kwa kasi na dakika ya 25 walipata bao la kuongoza kupitia penati iliyopigwa na Patrick Sibona
Mpaka mpira unakwenda mapumziko Yanga alikuwa akiongoza kwa bao hilo. Kipindi cha pili mambo yalibadilika na Zesco walirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi ambayo yalizaa goli dakika ya 90+5 lililofungwa na mchezaji aliyeihama timu hiyo Thaban Kamusako.

                                          Thaban Kamusako akishangilia bao dhidi ya Yanga
Baadhi ya wadau wamedai ,wachezaji wa Yanga walianza kupoteza muda ilihari wapo nyumbani na wanaongoza kwa bao moja tu.

Yanga inapaswa kujitathimini zaidi kuelekea mchezo wa pili utakaopigwa tarehe 27 jijini Lusaka na watakutana na upinzani mkali kwani Zesco ni moja ya timu nzuri hasa inapokuwa nyumbani.

Kama Yanga itashinda basi itafanikiwa kuingia hatua inayofuata(Makundi).

Sisi kama AMOSPOTI.COM  tunawatakia Yanga Sc maandalizi mema na tunaamini watafanya vizuri kwenye mchezo unaofuata.




Post a Comment

0 Comments