BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAFA KIBABE ZAMBIA

Klabu ya Yanga imeshindwa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika baada ya kuruhusu kipigo cha 2-1 dhidi ya Zesco.
Zesco ilionekana kuuanza mchezo huo kwa umakini na dakika ya 25 ilipata bao la kuongoza kupitia Jesse ware Yanga hawakuwa nyuma kwani dakika ya 31 waliinyamazisha Zesco kupitia Sadney Khoetage. Mpaka mapumziko Yanga 1-1 Zesco.

Kipindi cha pili timu hizo zilionyesha uwezo wa hali ya juu na Dakika ya 79 beki wa Yanga (Makame) alijifunga kwa bahati mbaya kupitia shuti kali la mchezaji wa Zesco.

Yanga imetolewa na Zesco kwa jumla ya mabao 3-2. Baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam kutoshana nguvu kwa bao 1-1.

Tanzania imekosa mwakilishi hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika hivyo mwakani itapeleka timu mbili tu badala ya nne kama msimu huu.

Post a Comment

0 Comments