ads

adds

YANGA BADO WAPO WAPO SANA KIMATAIFA

BAADA ya kikosi cha Yanga kupoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Zesco United sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye Kombe la Shirikisho.

anga ilitolewa na Zesco kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2 hivyo wanafungasha virago kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na kutupwa kwenye Kombe la Shirikisho.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa haikuwa malengo ya Yanga kufikia hatua hiyo ila ni matokeo haina budi kuyapokea.

"Kwa sasa sisi ni wa kimataifa, kushindwa kwetu kutinga hatua ya makundi haina maana ya mwisho wa mbio kimataifa bali tunaingia kwenye Kombe la Shirikisho huko tutapambana.

"Shukrani kwa mashabiki kwa sapoti kubwa na Yanga tumeonyesha maana ya kuwa wa kimataifa tumetoka kulia tumeingia upande wa kushoto," amesema.
29Sep2019



Next
This is the most recent post.

Post a Comment

0 Comments