Muingereza huyu amekuwa na msimu mzuri zaidi msimu huu baada ya kufunga Hat trick yake ya kwanza dhidi ya Wolves kwenye ushindi wa 5-2.
Tammy Abraham anaumri wa miaka 22 na ni zao la Academy ya Chelsea. Alianza kuaminika zaidi msimu wa 2016-2017 akipelekwa kwa mkopo klabu ya Bristol, msimu wa 2017-18 alipelekwa Swansea City na msimu wa 2018-19 alipelekwa tena kwa mkopo klabu ya Aston Villa. Akiwa katika vilabu hivyo alifanikiwa kufunga jumla ya magoli 60 katika mechi 116 alizocheza.
ABRAHAM AKISHANGILIA BAO DHIDI YA WOLVES
Mchezaji huyu chipukizi ameshaichezea timu ya Taifa Uingereza mechi na kufunga magoli 46 na kufunga magoli 16. Mwaka 2017 alicheza mechi 2 za timu ya wakubwa.
Mchezaji huyu kwa sasa anaongoza ligi kwa kuwa mfungaji namba moja akifuatiwa na Aguero wa Manchester City. Kwa takwimu zake Abraham anaonekana yupo vizuri na pia ni mchezaji mwenye uwezo wa kumiliki mpira,upigaji chenga na spidi .
Binafsi naamin msimu huu anaweza kufikisha zaidi ya magoli 15 na kama mambo yatamwendea vizuri pale darajani basi timu pinzani zijiandae kukumbana na maumivu.
2 Comments
asante kwa taarifa mkuu, nakupata kwa uzurii mnooo
ReplyDeletePamoja sana man
Delete