BETI NASI UTAJIRIKE

MCHUNGAJI WA YANGA AIBUKA NA LIGINE

Mchungaji mmoja afahamikae kwa jina la Mashimo amezua taharuki nyingine kwa wapenzi wa soka  baada ya kuomba sadaka kwa mkuu wa mkoa wa Kagera.

Msimu uliopita mchungaji huyo aliibuka na kusema Yanga atatwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara matokeo yake Simba ilinyakua ubingwa huo.

Msimu huu mchungaji ametoa maelezo mengine kwa mkuu wa mkoa wa Kagera kumpelekea mchungaji huyo sadaka ya pekee ili timu hiyo iweze kuifunga Simba kwenye mzunguko wa pili wa ligi.

Mchungaji huyo ameonekana akitumia vifungu vya biblia kumsistiza mkuu huyo wa mkoa na amesema endapo wasipotuma fedha hiyo basi mchezo wa marudiano watafungwa tena na Simba. Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa simba kuifunga Kagera Sugar  mabao 3-0 na mchezo wa marudiano utachezwa mwaka 2020.
 Msimu wa mwaka 2017/2018 Simba ilipoteza michezo yake kwa Kagera Sugar na mchungaji huyo anadai aliifanyia maombi timu hiyo kuweza kuifunga Simba.

Post a Comment

0 Comments