BETI NASI UTAJIRIKE

MAKAME UHAKIKA KIKOSI CHA KWANZA YANGA

Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amemuingiza rasmi kiungo wake mkabaji, Abdulaziz Makame kwenye kikosi chake cha kwanza atakachokitumia kwenye Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa Afrika.
Kauli hiyo aliitoa Jumamosi mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, bao la Yanga lilifungwa na Patrick Sibomana huku lile la Zesco likipachikwa na Thabani Kamusoko.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Zahera alisema kuwa alishindwa kumtumia kiungo huyo kwenye michezo iliyopita kutokana na kutokuwa fiti.

Zahera alisema bado anaendelea kumtengeneza kiungo huyo kwa kumpa mechi za mfululizo ili arejee katika kiwango ili awe bora zaidi ya alivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Zesco.

Aliongeza kuwa kinachomshawishi aendelee kumtumia kiungo huyo ni umbile kubwa alilonalo, pia aina yake ya uchezaji ya kugongana huku akitumia nguvu nyingi na akili.

“Kwenye mechi hii na Zesco katika dakika ya 70 nilipanga kumtoa Makame baada ya kumuona amechoka, lakini nilimbakisha baada ya kuona umuhimu wake wa kuokoa mipira ya juu ya kona, faulo.

“Lakini sikupanga kumtumia kwa dakika zote 90 kutokana na kukosa ‘match fitness’, Makame hakukaa na timu muda mrefu tangu ajiunge na Yanga, muda mwingi amekuwa na timu ya taifa, Taifa Stars.

“Hivyo hakupata mechi nyingi za kirafiki kama walivyokuwa wachezaji wenzake, hivi sasa ndiyo ninaanza kumjenga na malengo yangu ni kumuona akiwa bora katika kikosi changu cha kwanza,” alisema Zahera.

Post a Comment

0 Comments