advertise with us

ADVERTISE HERE

KILOMONI AICHOKONOA TENA SIMBA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini katika klabu ya Simba, Hamis Kilomoni, amemtaka Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji 'Mo' kuweka bilioni 20 katika akaunti ya klabu hiyo.
Kilomoni ameibuka na kauli hiyo baada ya Mo kushindwa kuweka fedha hizo hadi sasa ili ziweze kutumika ndani ya klabu kwa mambo mbalimbali.

Ameeleza anashangwaza na Mo kama ameamua kuwekeza kwanini asiweke fedha hizo kama kweli amewekeza na siku zinazidi kwenda.

Amefunguka akieleza kuwa yeye si kwamba anapinga Mo kufanya uwekezaji bali ni vema taratibu zote akazifuata na si kuitumia Simba kwa manufaa yake pekee.

"Ujue mimi nashangaa mpaka leo Mo hajaweka zile bilioni 20 alizoahidi mpaka leo.

"Nashangaa amekuwa kimya, kama amewekeza kwanini asiziweke kwenye akaunti ya klabu, ni uwekezaji gani huo?

"Mimi sipindi yeye kufanya uwekezaji, ninachotaka ni vema akafuata tu taratibu zinazototakiwa na kila mtu atamuunga mkono."

Post a Comment

0 Comments