Mchezo huo uliopigwa dimba la Kaitaba mkoani Kagera ulianza kwa kasi na dakika ya tano Simba walijipatia bao la kuongoza kupitia Meddie Kagere na dakika ya 27 Simba ilipata bao la pili kupitia kapteni wake Muhamed Hussein "Tshabalala" na kipindi cha kwanza kilikamilika kwa simba kuongoza mabao mawili . Simba walionekana kuukamia sana mchezo na kufanikiwa kuuvunja mwisho wa kufungwa na Kagera kwa kuongeza bao la tatu lililowekwa wavuni na Meddie Kagere.
Historia ya Patrice Aussen dhidi ya Kagera Sugar
Msimu wa 2017/18 Mchezo wa raundi ya kwanza ulimalizika kwa sare tasa na raundi ya pili Simba ilifungwa bao moja mchezo ulioshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli akiwa na msemaji wa Simba Haji Manara na naibu waziri wa Michezo Juliana Shonza
msimu wa 2017/18.
Msimu wa 2018/19 Simba ilipoteza michezo yote miwili kwa Kagera Sugar na kuendeleza uteja huo ingawa msimu huu imevunja uteja huo baada ya kushinda mchezo wake wa kwanza ikiwa ugenini Kagera.
0 Comments