advertise with us

ADVERTISE HERE

ALEXIS SANCHEZ NOMA, MANCHESTER UNITED INAUA VIPAJI

Mshambuliaji wa Manchester United aliye uhamishoni kwa mkopo klabu ya Inter milan amewashtua na kuwatibua Manchester United.


Mchezaji huyo alijiunga na Manchester mwaka 2017 na hakuwahi kuonyesha cheche zozote baada ya kufunga maoli matatu tu huku akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara .

Sanchez ndie mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa zaidi ligi kuu Uingereza lakini alishindwa kudhihirisha thamani ya fedha hizo ndipo mwanzoni mwa msimu huu alipelekwa Inter Milan kwa mkopo ambako ameungana na mchezaji mwingine wa Manchester United Romelu Lukaku.

Kwenye mchezo wa Serie A Sanchez alionyesha ubora wa hali ya juu baada ya kufunga magoli 2 kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Samporia. Suarez alifunga mabao hayo dakika ya 20 na 22 huku akipewa kadi nyekundu dakika ya 46 kipindi cha pili kwa kujiangusha ili apate penati.


Post a Comment

0 Comments