advertise with us

ADVERTISE HERE

PELLEGRIN: RONALDO NA MESSI WANATAKIWA KULIPWA SAWA

Kocha wa zawani wa klabu ya Real Madrid amesema Cristiano Ronaldo ni wachezaji wanaopaswa kulingana mishahara
 Ronaldo anamkataba na Real Madrid mpaka mwaka 2021, vyanzo vya ndani vinadai Ronaldo anataka kuongezewa mshahara zaidi baada ya  msimu uliopita kuisaidia timu hiyo kutwaa vikombe vitano vikubwa. na mshahara wake uko chini ya Lionel Messi na Neymar JR.
Vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vinasema Ronaldo anatamani kurejea klabu yake ya zaman Manchester United. Hivi Karibuni mchezaji huyo alisema anafuraha kuwepo Real Madrid na anadhani atakuwepo hapo kwa muda mrefu zaidi.
Pellegrin ndiye kocha aliyempokea Ronaldo kutokea Manchester United na sasa kocha huyo yupo China akiifundisha klabu ya Hebei China Fortune amesema "Messi anakipaji cha kuzaliwa na hakuna wa kumfananisha naye"
Pellegrin aliongeza " Ronaldo ni mchezaji anaejituma na kutambua wajibu wake awapo uwanjani hilo linamfanya awe bora, anaweza asifikie uwezo waMessi lakini amekuwa akijituma na kulingana kimafanikio na Lionel Messi"
"Naamini wote ni wachezaji wazuri na wanatakiwa kulipwa zaidi duniani" alimaliza Pelegrini

Kuhusu kuondolewa kwa Real Madrid katika michuano ya Copa Del Rey na Madrid kutofanya vizuri La Liga Pelegrin amesema " sishangazwi na mfumo wa soka miaka ya hivi karibuni, Zinedine Zidane ameshinda makombe mengi makubwa kwa kipindi kifupi , hilo ni jambo la kawaida ukiwa na timu nzuri pia kufanya vibaya hutokea hasa timu inapokuwa imeshinda makombe mengi"
" Real Madrid wanakikosi kizuri na wanaweza kufanya maajabu tena ligi ya Mabingwa Ulaya " alimaliza Pellegrin.

Post a Comment

0 Comments