BETI NASI UTAJIRIKE

SASA NI RASMI AUBAMEYANG NI MCHEZAJI WA ARSENAL

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amedhibitisha kumnasa Aubameyang kwa kitita cha paundi milioni 60.
 Kupitia  arsenal.com video fupi iliyofutwa baadae  ilionyesha timu hiyo imefanikiwa kumnasa staa huyo mwenye miaka 28 na Arsenal wanataka kumtambulisha kwa suprise. Hapo Jana picha zilisambaa mitandaoni zikimwonyesha Aubameyang akiwa uwanja wa ndege jijini Dortmund na ilifahamika anaelekea jijini London.
Aubameyang akiwasili Uwanja wa ndege jijini Dortmund.
Gari lililombeba Aubameyang alipokuwa amewasili jijini London.
Klipi iliyofutwa ilimhusu wenga na ripota wa klabu aliehoji
Ripota : " Pierre  Aubameyang ni mchezaji wa Arsenal , unazungumziaje uwezo wake?
Wenger: Ni habari nzri na tunahitaji wachezaji kama yeye wenye uwezo wa kutupa changamoto mpya za ushindani, mpaka sasa hatuwezi kwenda mbele ila naamini uwepo wake utasaidia"
" Kuna ushindaji mkubwa mbele yake na anataka kufanya vizuri katika ligi hii ni habari njema kwa klabu yetu , ni moja ya washambuliaji ambao naamini atafanya vizuri katika ligi , uwezo wake wa kukimbia , nguvu na umakini ni vitu pekee vinavyotakiwa ligi kuu Uingereza " alimaliza Wenger.
Aubameyang anaweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi katika kikosi cha Arsenal paundi milioni 60 baada ya Mesuit Ozil aliesajiliwa kwa paundi milioni 40.

Post a Comment

0 Comments