Klabu ya Arsenal imefanikiwa kumbakiza Mesuit Ozil kwa kumpa mkataba utakaomwingizia paundi 350,000 kwa wiki.
Kiungo huyo ameongeza mkataba wa miaka 3 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji anaelipwa zaidi klabuni hapo. Ozil alikuwa amebakiza miezi 4 tu ya kuichezea Arsenal na angeondoka bure majira joto.
Miezi kadhaa iliyopita Ozil alihusishwa na kuhamia Manchester United ama Barcelona.
Arsenal wamesema mkataba mpya bado haujasainiwa ila mazungumzo ya awali yalionyesha Ozil kuukubali mkataba huo. Mapema mwezi huu Wenger alisistiza kuwa Ozil ataongeza mkataba.
Arsenal wanaamini Jack Wilshere ataungana na Ozil kusaini mkataba mpya. Vyanzo vya ndani klabuni hapo vimesema Ozil anataka kuendelea kuishi jijini London na njia pekee ni kuongeza mkataba na klabu hiyo.
0 Comments