advertise with us

ADVERTISE HERE

STAA WA KWANZA DUNIANI KUMILIKI SHIRIKA LA NDEGE "BABY JET AIRLINE

Unaweza usiamini, ila ndivyo ilivyo kwa staa wa timu ya Taifa ya Ghana Asamoah Gyan ameanzisha shirika lake la ndege na litaanza kufanya kazi hivi karibuni.
 Asamoah Gyan alijiunga na Sunderland ya Uingereza akitokea Rennes kwa dau la Paundi milioni 13. aliichezea michezo 37 na kufunga magoli 11 kabla ya kutimkia falme za kiarabu na kujiunga na klabu ya AL AIN.aliondoka tena katika timu hiyo ya falme za kiarabu na kujiunga na klabu ya Shanghai SIPG ya China.Mambo hayakumwendea vizuri ndipo aliamua kujiunga na klabu ya Uturuki Kayserispor .
Rais wa Ghana Nana Akufo ndiye alietoa siri ya mchezaji huyo kuanzisha shirika lake la ndege.
"Nimeambiwa kapteni wa timu yetu ya taifa Asamoah Gyan amechukua leseni ya shirika lake la ndege na ameliita baby jet.Huu ni wito kwa waghana wote waliopo ndani na nje ya nchi kuwekeza katika nchi yetu" alisema Rais huyo.
Imefahamika mchezaji huyo ataanza kwa huduma ya kusafirisha mizigo kisha baadaye ataanza kubeba abiria. Gyan ni mchezaji wakwanza duniani kuwa na shirika binafsi la ndege na hiyo ni ishara soka linalipa .

Post a Comment

0 Comments