advertise with us

ADVERTISE HERE

RONALDO AMPIKU TENA LIONEL MESSI TUZO ZA FIFA

Nyota wa Real Madrid  Cristiano Ronaldo amefanikiwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa kiume ( FIFA BEST PLAYER) kwa mara ya pili mfululizo.
 Baada ya kuisaidia Real Madrid kushinda ligi ya mabingwa Ulaya na kuisaidi timu ya taifa Ureno Cristiano Ronaldo(32) ameibuka mshindi wa kwanza katika tuzo za mchezaji bora wa FIFA akiwamwaga Lionel Messi wa Barcelona na Argentina pamoja na Neymar wa Paris Saint-german na Brazil.
Kwa mara ya pili mfululizo Ronaldo amenyakuwa tuzo hiyo tangu ianzishwe mwaka 2016.
Kocha Bora amefanikiwa kuchukua Zinedine Zidane baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa makombe matatu msimu huu.

 kwa upande wa mchezaji  Bora wa wanawake Lieke Martens   wa Barcelona na Uholanzi alinyakuwa tuzo hiyo.
Kipa bora ilikwenda kwa Gianluigi Buffon wa Juventus na Italy  akiisaidia klabu yake kubeba ubingwa wa Italy mwaka  huu na kufika fainali za ligi ya mabingwa Ulaya kwa kufungwa magoli matano tu.
Mchezaji wa Arsenal na Ufaransa Olivier Giroud  amepata tuzo ya Puskas kwa goli bora aliloshinda dhidi ya Crystal palace mwezi Januari.
Mashabiki wa Celtic wameshinda kama mashabiki bora. Fifa wametangaza kikosi bira cha mwaka 2017. Real madrid imeongoza kwa kuwa na wachezaji watano (Cristiano Ronaldo,Toni kroos,Luka Modric na Ramos) Barcelona imemtoa (Lionel Messi na Andre Iniesta), PSG imemtoa (Neymar na Dani Alves) ,AC Milan imemtoa (Gianluigi Bonnuci)  na Juventus ikimtoa (Gianluigi Buffon). hakuna mchezaji wa Uingereza alietajwa.

Post a Comment

0 Comments