Nahodha wa Uholanzii Argen Robben amekata tamaa ya kushiriki kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018
Mbali na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Belarus Uholanzi inakutana na kikwazo kikubwa mbele yake dhidi ya Swedeni mchezo utakaopigwa jumanne hii mjini Amsterdam na itahitaji mabao 7-0 kuweza kufuzu michuano hiyo kitu ambacho ni kigumu zaidi kwa timu hiyo.
" inanipa wakati mgumu na maumivu pia ila huu ndio mpira "alisema mchezaji huyo wa Bayern munich alieichezea timu yake ya taifa michezo 95 akikaribia kustaafu.
Mechi ya jumamosi iliifanya timu hiyo kuwa na pointi 16 katika michezo 9 ya kundi A nyuma ya sweden yenye pointi 19 ikiwa na kuizidi uholanzi magoli 6.
Sweden ilishinda magoli 8-0 dhidi ya Luxemborg jumamosi iliyopita na Robben alisema "hatukutegemea kama watashinda magoli yale yote ila tunaamini mpira dakika 90 na lolote linaweza kutokea alimaliza robben
0 Comments