BETI NASI UTAJIRIKE

POGBA AONYESHA MATUMAINI KUREJEA DIMBANI HIVI KARIBUNI

Staa wa ufaransa na Manchester United amezidi kuonyesha matumaini kurejea dimbani baada ya kuonekana akiendelea vizuri  na mazoezi jijini Miami marekani.
Pogba yupo jijini Miami kwa mapumziko na matibabu ya majeraha baada ya kuumia dakika ya 12 katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Basel mwezi septemba 12
Pogba ameonyesha kumudu mazoezi anayopewa na walimu wawili wa viungo na  kuyamudu  hivyo kuifanya Manchester United  kuweka matumaini  kurudi mapema kwa mchezaji huyo.
Ndani ya siku 17 Manchester united  itakuwa na michezo 6 ya michuano tofauti na hilo limemwingiza hofu kocha Jose Mourinho . Marcos Rojo,Ibramovich na Pogba ni wachezji muhimu na wote wameonekana kuwa majeruhi. Mourinho amesema "majeraha ya pogba siwezi linganisha na ya wachezaji wengine, na siwezi sema ni maumivu ya muda mrefu ama la , pia sifikirii sana kwa hawa wachezaji kama ,Ibrahimovich, Rojo na hao wengine"
kwa upande mwingine kiungo mwenza wa Manchester united Nemanja Matic amesisitiza timu itacheza vizuri bila uwepo wa pogba.
"Tunajua atakuwa nje kwa kipindi flani,na ni mchezaji muhimu katika timu na tunaamini atarejea karibuni, Pogba ni mchezaji muhimu kwa timu ila tunawachezaji wengine wengi wanaoweza cheza nafasi yake" alisisitiza Matic

Post a Comment

0 Comments