advertise with us

ADVERTISE HERE

POCHETTINO; TUTAIFUNGA MANCHESTER UNITED BILA HARRY KANE

Kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino amesema wataifunga Manchester United bila ya uwepo wa nyota wao tegemezi Harry Kane.
 Harry Kane hatacheza mchezo wa leo dhidi ya Manchester United kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi yaWestham United na mchezo  ulimalizika kwa Tottenham kufungwa goli 3-2 na kutolewa katika mashindano ya Carabao Cup. Hilo ni pigo kwa Totenham kwani mchezaji huyo amekuwa akiongoza vyema safu ya ushambuliaji kwa kufunga magoli 8 katika mechi 9 za ligi kuu Uingereza.
 Pochettino ameongea kwa msisitizo kuwa atashinda mchezo huo bila ya mshambuliaji wake hatari Harry Kane  'Naamini tunaweza shind mchezo huu bila ya Harry Kane na tutatumia wachezaji tofauti, tumeshacheza michezo mingi bila ya Kane kwa sasa tuna Fernando. kama utakumbuka msimu uliopita tulimtumia Sonny wakati Kane akiwa majeruhi ni suala tu la kutafuta mbadala sahihi wa Kane" alisema Pochettino.
Baadhi ya waandishi walimuhoji Jose Mourinho kukosekana kwa Harry Kane dhidi ya timu yake Manchester United "siko hapa kuzungumzia wagonjwa wa timu nyingine , kwahiyo msiniulize kuhusu Harry Kane natakiwa niwazungumzie Pogba, Ibramovich, Marcos Rojo na Michael Carrick. Phil Jones alikosekana jumanne ila mchezo huu atakuwepo" alisema Mourinho

Post a Comment

0 Comments