kiungo wa Arsenal , Mesuit Ozil amezipinga vikali tetesi za kujiunga na klabu ya Manchester United mara baada ya kugoma kusaini mkataba mpya.
Habari za ndani zinasema mchezaji huyo amekuwa akiwaambia wenzake kutaka kucheza chini ya Kocha Jose Mourinho wa Manchester United.
Ozil amekanusha vikali tetesi za kujiunga na Machester United na amesema anataka aweke rekodi katika klabu yake ya Arsenal.
Rafiki wa karibu na Ozil alisema " kulikuwa na mazungumzo kati ya Ozil na Arsenal msimu uliopita mpaka mwezi machi kuhusu ongezeko la mshahara, lakini toka mwezi huo mazungumzo yalisitishwa"
Mesut Ozil ndiye mchezaji ghali zaidi kwa Arsenal alinunuliwa kutoka Real Madrid kwa dau la paundi milioni 42. nyota huyo analipwa kiasi cha paundi 170,000 kwa wiki na inasemekana anataka kulipwa kiasi cha Paundi 300,000 kwa wiki.
Mchezaji huyo mwenye miaka 29 anahusishwa kuwa na mazungumzo na kocha wa Manchester United Jose Mourinho.
Rafiki yake wa karibu anasema Ozil anataka kubaki jijini London, ingawa mkataba wake unaisha mwakani na Arsenal kushindwa kukubaliana na staa huyo ni dalili tosha Arsenal italazimika kumuuza kwa hasara ama kumtoa bure mwishoni mwa msimu.
0 Comments