advertise with us

ADVERTISE HERE

MOURINHO: NIPO TAYARI KUONDOKA MANCHESTER UNITED

Jose Mourinho ameweka wazi kutostaafu katika klabu ya Manchester United hivyo kuipa nafasi klabu ya Paris-saint German
Mbali na kuongezwa mkataba wa miaka mitano na klabu ya Manchester United .Mourinho amekiri kuto kuwa na maisha marefu na klabu hiyo ya uingereza. hayo yamefahamika leo alipoulizwa na kituo cha Ufaransa kama atakataa tena ofa ya kuifundisha PSG baada ya kukataa kujiunga na klabu hiyo mara mbili .
 
Mourinho alisema " mimi ni kocha mwenye mipango, na napenda kujaribu vitu vipya sidhani kama nitamaliza maisha Manchester United".
kocha huyo alikwenda mbali zaidi kwa kuipongeza PSG na kisema hata mtoto wake huenda kuitazama klabu hiyo inavyocheza na si Manchester United.
 Mashabiki wa Manchester wanaungoja kwa hamu  mtanange dhidi ya magwiji hawa wawili na wengi wamekuwa wakitoa maoni tofauti kutokana na makocha hawa kuanza msimu vizuri .
 Manchester city inayonolewa na Guardiola inaongoza ligi kwa point 22 ikiwa imecheza mechi nane kufunga magoli 29.na kuruhusu magoli 4 na mechi moja kudroo.
Manchester  United imecheza michezo 8 ikishinda 6 na kudroo 2 ikishinda magoli 21 na kufungwa magoli  2 na kuwa na pointi 20.
Mahasimu hawa watakutana tarehe 9 mwezi Disemba.
Mourinho ameonekana kuanza vizuri tangu atue Manchester United kwa kuisaidia klabu hiyo kubeba makombe matatu ndani ya miezi 16 na kufanya vizuri mechi 10 za michuano mbalimbali bila kufungwa hata moja.
Jumatanio hii Manchester United inakutana na Benfica katika mchezo wa klabu bingwa ulaya

Post a Comment

0 Comments