advertise with us

ADVERTISE HERE

MANCHESTER UNITED, REAL MADRID NA BARCELONA ZAMTOLEA MACHO OZIL

Manchester United haijafanikiwa kuanza mazungumzo na Ozil anaetaka kuondoka Arsenal msimu huu baada ya klabu yake kushindwa kukidhi matakwa ya mkataba wake.
 Barcelona na Real Madrid nao wameonekana kumtaka Ozil mwenye miaka 29. Staa huyo anataka mshahara wa paundi 200,000 kwa wiki ili aweze kuendelea na miamba hiyo ya London.
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anapewa nafasi kubwa kumchukua staa huyo kutokana na kuwa na mawasiliano mazuri na mchezaji huyo tangu walipokuwa Bernabeu.
 Manchester United imekuwa na kawaida ya kuwalipa vizuri wachezaji wake na kiasi cha paundi 200,000 kwa wiki si tatizo kumpa Ozil.
vyanzo vya karibu na Ozil vinasema"Tunafahamu anamawasiliano na Mourinho na anapenda kucheza chini ya Mourinho.anasema ni kocha mzuri kuwahi kufundishwa nae pia wana uhusiano mzuri".
Endapo Arsenal itashindwa kumuuza mchezaji huyo mwezi Januari itamwachia aondoke bure mwishoni mwa msimu huu.
Wenger atakutana na wakati mgumu kumuuza mchezaji huyo kwa mpinzani wake Jose Mourinho


Post a Comment

0 Comments