advertise with us

ADVERTISE HERE

CHELSEA YAPATA KOCHA MPYA, KURITHI MIKOBA YA CONTE

Mabosi wa Chelsea hawavutiwi na mwenendo wa timu na sasa wanataka kumfukuza kocha Antonio Conte.
 Tetesi zinasema mbadala wa kocha huyo ameshapatikana na aliwahi ifundisha na kuisaidia Chelsea kutwaa mataji kadhaa
Bodi ya mabosi wa Chelsea imekuwa na kawaida kufukuza makocha pindi tu wanaposhindwa kufanya vizuri. Conte alichukua nafai ya Jose Mourinho kutokana na kocha huyo kushindwa kutetea ubingwa na sasa ni zamu ya Conte kuondoka.
Carlo Ancelloti anatajwa zaidi kuchukua nafasi ya Conte. kocha huyo amekuwa na mahusiano mazuri na Chelsea tangu mwaka 2011 alipotimuliwa. amezifundisha  Real Madrid ,PSG na Bayern Munich na sasa anatazamiwa kuifundisha tena  Chelsea.
 Msimu wa 2010/11 alifanikiwa kubeba mataji mawili makubwa EPL na FA lakini mwanzoni mwa mwaka 2011/12 alifukuzwa kwa kuanza vibaya msimu huo na nafasi yake kuchukuliwa na Andre Villas Boaz.  Ancelotti yupo jijini London na anahusishwa zaidi kujiunga na klabu hiyo.

Post a Comment

0 Comments