ads

adds

GHANA KUKATA RUFAA FIFA DHIDI YA UGANDA

Chama cha soka nchini Ghana GFA kimekata rufani FIFA  dhidi ya Uganda wakitaka mchezo huo urudiwe .
 Ghana walielekea Uganda kwa nia moja tu ya kushinda mchezo huo lakini hali ilikuwa ni tofauti kwani mpaka filimbi ya mwisho timu hizo hazikufanikiwa kufungana na kuipeleka Ghana nafasi ya tatu inayoiondoa timu hiyo kuendelea na kinyang'anyiro kushiriki kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
Chama cha soka la Ghana kimesema kiliiandikia FIFA barua kuhusiana wachezeshaji wa mchezo huo refarii Daniell Bennett na wasaidizi wake Adelaide na Steve Marie waliochezesha  mchezo dhidi ya Afrika kusini.
chanzo cha ndani kinasema GFA walituma barua barua FIFA mara baada ya mchezo dhidi ya Uganda barua hiyo inasema "Refa Bennett na wasaidizi wake walikataa goli katika dakika ya 93 ilihali televisheni ilionyesha ni goli sahihi"
ghana ilikataliwa penati katika kipindi cha kwanza hali iliyozua maswali mengi  na maamuzi mengi yakipingwa na waamuzi hao.kilisema chanzo hicho. pia kiliongeza
"tunaheshimu maamuzi ya FIFA ila tunaomba mechi hiyo iweze kurudiwa kuzuia mitafaruko na kuweka mambo sawa" kilimaliza chanzo hicho

Post a Comment

0 Comments