advertise with us

ADVERTISE HERE

CRISTIANO RONALDO AMFUNIKA TENA LIONEL MESSI

Jarida la Forbes 2017 limetoa orodha ya wanamichezo wanaolipwa zaidi kwa mwaka 2017. nimekusogezea hapa listi ya wanamichezo watano.
1.Cristiano Ronaldo 
 Ronaldo ndiye mchezaji alieongoza kulipwa msimu huu kwa kuingiza kiasi cha dola milioni 93. chanzo cha mapato ni mshahara wake wa dola milioni 55 akiwa mchezaji tegemezi wa Real Madrid na Portugal. pia analipwa kiasi cha  dola milioni 38 kupitia mikataba ya matangazo.
2. LeBron James
Ndiye mchezaji namba moja kwa upande wa kikapu (NBA) akishikilia nafasi ya pili nyuma ya Ronaldo. chanzo cha mapato yake ni mshahara wa dola milioni 31.2 na mikataba ya matangazo kiasi cha dola milioni 55. hii inamfanya mchezaji huyu kukusanya kuasi cha dola milioni 86.2 kwa mwaka.
3.Lionel Messi
 Mchezaji bora duniani mara 5 Lionel Messi anakamata nafasi ya tatu nyuma ya mpinzani  wake Cristiano Ronaldo. Messi anaingiza jumla ya kiasi cha dola milioni 53 mshahara kutoka FC Barcelona na kiasi cha dola milioni 27 kupitia mikataba ya  matangazo. jumla ya mapato kwa mwaka ni dola milioni 80.
4.Roger Federer
Mchezo wa Tennis unamfanya Federer kuwa namba 4 kwa kulipwa zaidi mwaka 2017. mswaziland huyu anaingizia kiasi cha dola milioni 6 kama mshahara wake kwa mwaka na kiasi cha dola milioni 58 kupitia mikataba ya matangazo. anapokea jumla ya dola milioni 64.
5. Kelvin Durant
 Umahiri wake katika mpira wa kikapu umemfanya Durant kushika nafasi ya pili kwa malipo akiwaburuza mastaa kibao wa NBA. Durant analipwa kiasi cha Dola milioni 26.6 kama mshahara na kiasi cha dola milioni 34 kupitia matangazo. kwa mwaka 2017 ameingiza kiasi cha dola milioni 60.4
Hakuna mchezaji yeyote wa Uingereza alieingia katika listi ya wachezaji wanaoongoza kulipwa mwaka 2017.

Post a Comment

0 Comments