advertise with us

ADVERTISE HERE

REAL MADRID: TUKIMKOSA HARY KANE TUNAMCHUKUA RASHFORD

Mabingwa wa Ulaya Real Madrid wameonyesha nia ya kumtaka Harry Kane baada ya  mchezaji huyo kuonyesha kiwango kikubwa misimu mitatu mfululizo.
 Real Madrid inaamini kumpata mfungaji bora wa EPL misimu miwili mfululizo 2015/16 na 2016/17. Msimu huu Kane  ameuanza vizuri. taarifa za ndani zinasema mchezaji huyo akishindwa kubeba kombe lolote kubwa msimu huu basi atalazimika kuondoka Totenham na kujiunga na klabu yoyote kubwa itakayofikia dau lake.
kwa upande mwingine habari za ndani kutoka Real Madrid zinasema klabu hiyo ipo tayari kumwaga kiasi kikubwa cha pesa ili kumpata kinda mashuhuri wa Manchester United na Uingereza Marcos Rashford. Florent Perez anahangaika kutafuta wachezaji vijana zaidi baada ya wachezaji wengi wa sasa kuwa na umri mkubwa na ameshaanza tafuta mbadala wa nyota hao.
Real Madrid wanataka kuwatumia Gareth Bale na Karim Benzema kama chambo kumnasa Kane au  Rashford na imeandaa kiasi cha Euro milioni 172 kumshawishi mchezaji Kane aweze kujiunga na miamba hiyo ya Ulaya. hilo limeonekana kuwezekana kwani klabu hizo zinauhusiano mzuri kibiashara .baada ya kumuuza  Modric na Gareth Bale alieweka rekodi ya uhamisho kabla rekodi yake haijavunjwa na Neymar, Tottenham itampoteza tena Harry Kane.

Post a Comment

0 Comments