advertise with us

ADVERTISE HERE

WENGER:KWA NINI UMEONDOKA BARCELONA

Arsene wenger amedhihirisha kusikitishwa na uamuzi wa neymar kuondoka Barcelona na kujiunga na PSG

                                               kocha wa Arsenal Arsene Wenger
Kocha huyo wa Arsenal ya uingereza amehoji ni kipi kimesababisha neymar kuikacha barcelona ?.  kwa upande wa neymar hajatoa jibu lolote lililopelekea yeye kuihama timu hiyo  hivyo amospoti.com limejaribu kukupa sababu za neymar kuondoka Barcelona .
fahari wawili hawakai zizi moja na hili linaweza kuwa jibu sahihi kwa kocha arsene wenger aliehoji kuondoka kwa mchezaji huyo  katika timu yenye wachezaji bora kabisa na kujiunga na psg ya ufaransa.

suala la kuihama klabu hiyo ya hispania limeonekana kumkera  Arsene Wenger kocha wa Arsenal ya uingereza huku dau alilonunuliwa Neymar  pauni millioni 222 na psg  kuzidi kumchefua zaidi.
                                                                        Neymar 

kama tunavyofahamu kila mtu hupenda kucheza katika timu yenye mastaa wakubwa. Neymar kaondoka Barcelona kwa mambo mawili makubwa .kwanza hakupenda kuwa chini ya Lionel Messi  mchezaji bora wa Dunia mara 5 hii itazidi kumfanya aonekane mchezaji wa kawaida akiwa Barcelona na dunia mbele ya Messi . Pia  ikumbukwe pindi Messi akiwa na umri wa miaka 23 alishakuwa mchezaji bora wa dunia wakati Neymar katika umri wa miaka 25 hajashinda tuzo.

sababu kubwa ya pili  ni fedha anayolipwa kwa wiki akiwa psg, kitita cha Tsh bilioni 1.6 anazolipwa Neymar ni ushawishi mkubwa kwa mchezaji yeyote hasa alietokea maisha ya kimaskini kama neymar.

mpaka sasa neymar ameshafunga magoli 4 katika mechi 4 alizocheza  huku akisaidia upatikanaji wa magoli 4 katika ligi kuu ufaransa (Ligue 1) .

Hapo kesho neymar atawaongoza wenzake katika  mechi ya ligi ya mabingwa ulaya UEFA  dhidi ya celtic . Je neymar atafanya makubwa katika mashindano haya ?


Post a Comment

0 Comments