BETI NASI UTAJIRIKE

TUPA KULE COSTA MORATA YUPO

Mashabiki wa chelsea wameanza kuwa na jeuri baada ya Morata kuopiga hat trick  dhidi ya Stoke city wikiendi hii .
 Mchezaji huyo aliesajiliwa akitokea Real Madrid amefunga Hatrick dhidi ya Stoke city na kuwa mchezaji wa pili kufunga hat trick. Morata anafungana na Romelu Lukaku  na Diego Costa  wote wakiwa na magoli 6 katika michezo 6 ya ligi.

Mastaa Johnstones wa Manchester city  na beki wa Chelsea Cahill hawakuficha hisia zao kwa kumpongeza mchezaji huyo kupitia instagram
Mashabiki wa Chelsea walionekana kumponda Diego Costa alierejea Atletico Madrid kwa kusema Costa ndio nani tuna morata.
kwa upandemwingine Diego Costa ameonekana jukwaani kwa mara ya kwanza kushuhudia timu yake mpya Atletico Madrid ikishinda goli mbili dhidi ya Sevilla.
costa hataichezea klabu hiyo mpaka mwezi january kutokana na klabu hiyo kufungiwa kusajili
Costa amesema "imechukuwa muda mrefu kwa mimi kuwa hapa lakini sasa tumekamilisha,  kwa sasa nitakuwa nikifanya mazoezi na kutazama michezo tu,. sikupenda nimalizane na chelsea vibaya na nilikuwa na uhusiano mzuri na kila mtu, mimi si mtu wa kuondoka kwa namna ile, nikweli nilikuwa nataka kurudi lakini kwa usajili wa kawaida , chelsea ni klabu kubwa ila Atletico ni nyumbani"

Post a Comment

0 Comments