Mchezaji Tammy Abraham anayeichezea timu ya Uingereza chini ya miaka 21 amekana kujiunga na timu ya taifa Nigeria
Tammy Abraham mzaliwa wa Uingereza lakini ana asili ya Nigeria kupitia baba yake ameitosa timu ya Taifa nigeria na kusisitiza atakipiga katika timu ya taifa Uingereza.
Mchezaji huyo wa Chelsea alie kwa mkopo katika klabu ya Swansea amefunguka hivi karibuni na kuweka misimamo yake baada ya vyombo vya habari kuripoti mchezaji huyo kuitosa Uingereza na alisema " Napingana na taarifa zilizolipotiwa na vyombo vya habari na ningependa kufafanua sijakubaliana na yeyote kuondoka timu ya taifa"
Abraham aliendelea kwa kusema "naweza kusema nilikutana na raisi wa NFF (Nigeria Football Federation) chama cha soka nigeria mara baada ya kumaliza mchezo wetu dhidi ya Tottenham na yeye ni rafiki wa baba yangu"
"Kama kutakuwa na mapendekezo yoyote ya mimi kubadili uraia wangu basi hiyo si kweli' alisema Abraham na kumalizia kwa kusema " nimezungumza na chama cha soka uingereza FA kwamba nipo tayari kuchaguliwa na timu ya taifa"
0 Comments