ads

adds

DAVID DE GEA KUBAKI MANCHESTER

Manchester United inajiandaa kumpa mkataba wa kudumu kipa David De Gea kuua dili la Real Madrid kumuwinda mchezaji huyo

Manchester United inajiandaa kufanya mazungumzo na David De Gea na wakala wake jinsi ya kumuongeza mkataba mchezaji huyo. Mkataba wa sasa unakwisha mwaka 2019 na Manchester United  inafanya jitihada kumzuia mchezaji huyo anaefuatiliwa na Real Madrid.
  Jose Mourinho na Manchester united wanaamini mchezaji huyo mwenye miaka 26  ataongeza mkataba na kubaki na timu hiyo.
De Gea alisajiliwa na kocha Alex Ferguson mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid na amezidi kuongeza uwezo siku hadi siku kwa kufikisha clean sheet 100 katika mchezo dhidi ya  Everton  waliposhinda goli 4-0

Real Madrid imehusishwa kumtaka kipa huyo tangu mwaka 2015 na manchester imekuwa ikimzuia kuondoka kutokana na umahili waake langoni na kuwa  mchezaji tegemezi zaid katika timu hiyo.

Post a Comment

0 Comments