ads

adds

MAKALA : MAMBO YA KUSISIMUA KUHUSU ‘FRENCH LEAGUE 1’

Wakati ligi mbalimbali za Ulaya zinaanza mwezi huu, macho na masikio mengi ya wanasoka yanaelekea pale Epl na Hispania, ila wanasahau ligi zingine kubwa. Kumbuka unapotaja ligi kubwa Ulaya huwezi kuitelekeza ligi ya Ufaransa maarufu kama ‘French league 1’ kutokana na umaarufu na ushindani wa ligi hii nalazimika kukuvuta kusudi uweze kufahamu mambo mazuri ambayo pengine hukuwahi kufahamu kwenye ligi hii yenye wachezaji wengi wa Kiafrika. Japokuwa yapo mengi ila leo fahamu haya machache Karibu tuwe wote hapa chini… French league 1 kwa mara ya kwanza msimu uliopita ilitoa timu ambayo iliongoza duniani kwa kuwa wastani mkubwa wa kuwalipa wachezaji. Psg ilikuwa na wastani wa Euro 5.3 Millioni kwa mwaka na kuongoza duniani kwa mujibu wa {Global sports salary} 2015, kiwango hiki ni sawa na wastani wa Euro 101,898 Miloni kwa mwezi Olympic Lyon bado inashikila rekodi ya kuchukua ubingwa wa League 1 mara 7 mfululizo, kumbuka tangu 2001 hadi 2007 wao ndo walikuwa wanachukua ubingwa huo. Kabla ya hapo walikuwa hawajawahi kuchukua ubingwa wa League 1. Marseil bado inaongoza kuchukua ubingwa huo mara nyingi, ikumbukwe imechukua mara 10 huku wakiwa washindi wa pili mara 12. Juninho ni miongoni mwa wachezaji waliochukua vikombe hivi mfululizo. Uwanja wa Stade Velodrome ambao msimu uliopita ulikuwa unatumiwa kama maskani ya Olympique de Marseille ndio uwanja mkubwa kuliko wote katika ligi kuu ya Ufaransa, uwanja huu unachukua watazamaji 67,344 ila cha kushangaza ni kwamba haujawahi kuwa ‘full’ na kujaza watazamaji wote tangu uongezwe ukubwa ili kuweza kutumika kwenye michuano ya ijayo ya Euro. As Monaco ndiyo timu pekee kutoka taifa huru ambayo inashiriki ligi kwenye nchi nyingine katika ligi ya Ufaransa. Kumbuka Monaco ni nchi huru yenye utawala wake ila kutokana na kutokusajiliwa na kukubaliwa na Uefa, waliomba kuwa miongoni mwa timu zinazowakilisha nchi ya Ufaransa kwenye michuano mbalimbali, ikumbukwe hata Swansea na Cardiff wanashiriki michuano ya England ila wanatoka nchi nyingine. Tangu mwaka 2000, Lyon na Psg ndizo timu ambazo zimetoa wafungaji bora kwa rekodi ya kushangaza kwani mara hizo zote kila mchezaji ameongoza mara mbili mfululizo, mfano Sonny Anderson {Lyon 2000 na 2001}, Pedro Pauleta {PSG, 2006 na 2007} Zlatan Ibrahimovich {2013 na 2014} Je Lacazzete naye atafanya hivo mara nyingine na kuendeleza rekodi hii? Alexandre lacazette alifunga magoli 27 msimu uliopita na kuwa mfungaji bora wa Erech League 1 huku akiwa ni mchezaji wa 4 kutoka Lyon kuchukua tuzo hiyo tangu timu hiyo ianzishwa miaka 116 iliyopita. Tangu kuanzishwa kwa tuzo za mchezaji bora chipukizi Frech league 1 imetoa wachezaji wawili pekee waliotwaa tuzo hiyo, Kareem Benzima 2008 na Eden Hazard 2011. Ikumbukwe tuzo hizi zilianzishwa mwaka 1978. Jean Pierre Papin, mchezaji bora wa zamani wa ulaya ndiye mchezaji anaeshikila rekodi ya kuwa mfungaji bora wa ligi mara 5 mfululizo wakati akiwa na klabu ya Olympic Marseyl. Kumbuka alistaafu soka mwaka 2001

Post a Comment

0 Comments