SIMBA YAJIANDAA VYEMA KUIKABILI SINGIDA UNITED LEO


Mabingwa wa nchi Simba leo wanawakaribisha Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Uhuru majira ya saa 10 jioni.Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya watani zao Yanga, kwa Simba huu ni mchezo muhimu kuondoka alama zote tatu

Katika mechi 11 zilizobaki Simba inahitaji kushinda michezo saba, hesabu inaanzia kwenye mchezo huu.Vijana wa Sven vandenbroeck walifanya mazoezi ya mwisho jana kwenye uwanja wa Mo Simba Arena tayari kuwakabili vibonde hao wa Ligi kuu ambao wanashika nafasi ya mwisho wakiwa na alama 12

Pengine kalamu ya mabao inaweza kushuhudiwa pale dimba la Uhuru
Kocha Sven huenda akawapumsidha baadhi ya nyota wake ambao juzi walicheza dhidi ya Yanga


Post a Comment

0 Comments