Arsenal wanawania kumnunua mlinda mlango wa Espanyol Mhispania Joan Garcia, 23, huku mlinda mlango wa Uingereza Aaron Ramsdale, 26, akitarajiwa kujiunga na Southampton kwa £25m. (Athletic -usajili unahitajika)
Mshambulizi wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, ambaye analengwa na Chelsea, amepewa mkataba wa miaka minne wenye thamani ya £25m kwa mwaka na klabu ya Al-Ahli ya Saudi Pro League . (Sky Sports)
Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, anatazamiwa kuhamia Juventus kutoka Manchester United kwa mkopo. (RMC Sport)
Aston Villa itamnunua mshambuliaji wa Roma ya Uingereza Tammy Abraham, 26, ikiwa mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 20 ataondoka katika klabu hiyo kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji . (Footalball Insider)
Crystal Palace wamekubali mkataba na Wolfsburg kwa mlinzi wa Ufaransa Maxence Lacroix, 24, kama mbadala wa moja kwa moja wa kiungo wa kati wa Denmark Joachim Andersen, 28, ambaye amejiunga na Fulham. (Sky Sports), nje
Liverpool wamekataa ombi la Bayer Leverkusen la kumnunua kiungo wa kati wa England chini ya umri wa miaka 21 Tyler Morton, 21. (Sky Sports)
Newcastle United wanataka kumsajili mlinda mlango wa Burnley wa England chini ya umri wa miaka 21 James Trafford, 21. (Football Insider)
Everton wamemuulizia kiungo wa Fiorentina kutoka Morocco Sofyan Amrabat, 28, ambaye alicheza kwa mkopo Manchester United msimu uliopita. (Talksport)
Uwezekano wa mshambuliaji wa Galatasaray na Ivory Coast Wilfried Zaha kurejea kwenye Ligi ya Premia umeondolewa kwa sababu ya masuala ya kodi. Klabu ya zamani ya Zaha Crystal Palace ilikuwa miongoni mwa wale wanaotaka kumsajili tena kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31. (Standard)
Beki wa Manchester City wa Burkina Faso Issa Kabore, 23, anatazamiwa kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda Benfica. (Sky Sports)
Fulham wana nia ya kumsajili winga wa Lyon mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ghana Ernest Nuamah. (Athletic – usajili unahitajika)
Wakati huo huo, beki wa Fulham ya Uswizi Kevin Mbabu, 29, anatazamiwa kujiunga na mabingwa wa Denmark FC Midtjylland kwa kandarasi ya miaka miwili. (Standard)
Winga wa Wolves wa Ureno Daniel Podence, 28, anakaribia kujiunga na Al-Shabab katika Ligi ya Saudia Pro League. (Rudy Galetti)
Nottingham Forest imekataa ofa kadhaa za mkopo kwa mlinda mlango wa Marekani Matt Turner, 30, kwa kuwa wangependelea aondoke kwa mkataba wa kudumu. (ESPN)
West Bromwich Albion na Burnley wanamuwania winga wa Celtic wa Jamhuri ya Ireland Mikey Johnston, 25, ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Baggies msimu uliopita. (Express & Star)
0 Comments