Klabu ya Namungo imeridhia maombi ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu Bw.Omar Kaya. Matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mechi mbili za ligi kuu NBC dhidi ya Tabora United mchezo ambao walipoteza kwa mabao 2-1 na kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gates.
Namungo inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa haina alama na kufungwa jumla ya mabao 4 katika mechi mbili walizocheza. Kikosi cha Namungo kipo chini ya kocha Mwinyi Zahera na kimesheheni wachezaji wazoefu wa Ligi kuu ya NBC akiwemo Kakolanya,Erasto Nyoni,Lenny Kisu,Jacob Masawe ,Frank Domayo na Emanuel Asante.
Hii hapa ni barua ya Afisa Mtendaji huyo
0 Comments