BETI NASI UTAJIRIKE

AZIZ KI AWEKA REKODI TUZO ZA TFF

 Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza rasmi tarehe na majina ya wachezaji mbalimbali walioingia kuwania tuzo mbalimbali za mwaka wa mashindano 2023/24. Katika Orodha hiyo jina la Aziz ki limejitokeza mara nyingi zaidi kushinda mchezaji yeyote aliyeshiriki ligi msimu huu.

Jina la Aziz Ki limejitokeza kwenye nafasi ya Ufungaji Bora wa NBC, Kiungo Bora NBC na mchezaji bora wa NBC lakini pia Azizi Ki ametajwa kuwania nafasi ya mchezaji bora wa kombe la CRDB. Kwa upande wa vilabu klabu ya Yanga imefanikiwa kutoa nyota 6 akiwemo Clement Mzize,Aziz Ki, Djigui Diarra,Ibrahim Bacca,Dickson Job ,Yao Kwasi pamoja na kocha Miguel Gamondi.

Azam FC wamefanikiwa kutoa wachezaji kama Feisal Salum,Kipre jr na kocha Bruno Ferry.kwa upande wa Simba wao wamefanikiwa kuwatoa wachezaji wawili pekee ambao ni kipa Ayoub Lakred na Mohammed Hussein.

Tuzo hizo zimepangwa kufanyika usiku wa  tarehe 1 Agosti katika ukumbi wa The Super Dome masaki jijini Dar es salaam .Hii hapa ni orodha ya wachezaji wote wanaowania tuzo mbalimbali zilizotangazwa.







Post a Comment

0 Comments