BETI NASI UTAJIRIKE

RASMI MBAPPE AMETANGAZA KUONDOKA PSG

 Kylian Mbappe ametangaza rasmi kuondoka PSG mara baada ya msimu wa 2024/25 kumalizika. Nyota huyo ameduumu ndani ya kikosi hicho kwa misimu 7 na sasa anatafuta changamoto mpya nje ya Ufaransa.

Kupitia video aliyoweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii Mbappe amenukuliwa akisema

 "Mkataba wangu unamalizika siku chache zijazo ndani ya PSG ,natangaza rasmi msimu huu ni wa mwisho na sitaongeza mkataba"

"ntacheza mchezo wangu wa mwisho siku ya jumapili katika dimba la Parc des Princes. kwa kipindi kirefu nimekuwa nikipata heshima ndani ya klabu hii kubwa Ufaransa na dunia kwa ujumla na ni sababu ya mimi kuwa hapa nilipo.nilipitia changamoto chanya kama mchezaji ,nikakutana na watu wazoefu na wenye  historia kubwa duniani ikanifanya nizidi kukua zaidi.

JE MBAPPE ANAONDOKA BURE NDANI YA PSG?

Mwaka 2021 Agosti Real Madri walitoa ofa ya kumtaka nyota huyo kwa kiasi cha dola milioni 220 lakini ofa hiyo ilikataliwa na na matajiri hao wa Paris na nyota huyo aliongeza mkataba wa miaka mitatu unaomalizika mwaka 2024.

PSG ilipokea na kukubali ofa ya kiasi cha Euro milioni 300 kutoka Al Hilal ya Saudi Arabia lakini nyota huyo alikataa kujiunga na miamba hiyo ya Saudi Arabia.

Mkataba wa Mbappe na PSG unakipengele cha makubaliano kwamba nyota huyo hataondoka bure bali atatoa GAWIO la usajili  kwa klabu ya PSG.Kuondoka kwa Mbappe ndani ya PSG kutapunguza gharama za uendeshaji wa klabu hiyo.

MBAPPE ANAELEKEA WAPI

Mbappe mwenye miaka 25 anahusishwa kujiunga na Real Madrid kwa msimu wa 2024/25. Taarifa zisizo rasmi zinasema nyota huyo amekwisha anza mazungumzo na miamba hiyo ya Hispania na mshahara wake umepunguzwa tofauti na ule uliopendekezwa mwaka 2021 alipotakiwa na klabu hiyo kwa kiasi chaa dola milioni 202 ambazo zilikataliwa na PSG. mpaka sasa klabu ya Real Madrid haijasema lolote kumhusisha nyota huyo lakini taarifa za ndani zinasema Mbappe atatambulishwa rasmi mara baada ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Dortmund.

nyota huyo anaondoka PSG akiweka historia binafsi na historia kwa klabu hiyo. hizi hapa ni takwimu za nyota huyo

Mbappe ndiye mchezaji nambari 1 kwa wingi wa magoli ndani ya PSG 


Mbappe akiwa na PSG amefanikiwa kuipa klabu hiyo jumla ya mataji 12 kwa kipindi cha miaka 7 


Post a Comment

0 Comments