JURGEN KLOPP ANAONDOKA KIFALME NDANI LIVERPOOL

 Kocha Jurgen Klopp ameaga na kuondoka rasmi Liverpool. Kocha huyo alijiunga na majogoo hao wa jiji mwaka 2015 akitokea Borrusia Dortmund. hili ni pigo kwa mashabiki wa Liverpool na  ligi ya Uingereza kwani uwepo wake ulirejesha hali ya ushindani wa Liverpool katika ligi hiyo .


Klopp anaondoka ndani ya Liverpool kwa  kutwaa kombe la ligi na amekosa makombe ya EPL ,FA na Europa. 

Tangu kocha huyo alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2015 alifanikiwa kutwaa jumla ya makombe 7 makubwa. Msimu wa 2018/19 Klopp alitwaa taji lake la kwanza la ligi ya mabingwa ulaya (UEFA) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs. Liverpool wamefanikiwa kufika hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mara 3 wakiwa na Klopp na fainali mbili walipoteza dhidi ya Real Madrid mwaka 2018 na 2022

Msimu wa 2019/20 Liverpool walifanikiwa kutwa a ubingwa wao wa kwanza wa EPL kwa kipindi cha miaka 30 na kurejesha hali ya matumaini ndani ya klabu hiyo.

Makombe mengine ambayo klabu hiyo imefanikiwa kutwaa chini ya Jurgen Klopp ni FA msimu wa 2021/22

Mwaka 2019 Liverpool walifanikiwa kutwaa ubingwa wa CLub World Cup dhidi ya Flamengo (1-0)

Mwaka 2019 walifanikiwa kutwaa kombe la UEFA Super Cup baada ya kuwaadhibu chelsea kwa mabao 5-4 kwa mikwaju ya penati.

msimu wa 2021/22 na 2023/24 Liverpool ilifanikiwa kutwaa kombe la ligi.

Klopp ameiongoza Liverpool kwa jumla ya michezo 491 na kushinda michezo 266 na kumfanya kuwa na wastani wa asilimia 60.9%  za ushindi zaidi ya kocha yeyote aliyewahi kuifundisha Liverpool.

Klopp ameiongoza Liverpool kufunga mabao 900 katika michezo 440 ikiwa ni michezo michache zaidi dhidi ya kocha wa zamani wa klabu hiyo Bill Shanky aliyefikia rekodi ya mabao 900 katika mechi 498

Msimu bora wa kukumbukwa zaidi kwa Klopp ni 2019/20 baada ya kumaliza ligi wakiwa na alama 99 na nafasi ya pili ilishikiliwa na Manchester City waliokuwa na alama 83.


Post a Comment

0 Comments