BETI NASI UTAJIRIKE

CHELSEA KUSHIRIKI MICHUANO YA ULAYA MSIMU UJAO

 Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brighton.Mabao ya Chelsea yaifungwa na Cole Palmer dakika ya 34 na bao la pili likifungwa na Christopher Nkunku dakika ya 64. bao la kufutia machozi kwa upande wa Brighton liliwekwa kimiani na Dani Welbrck dakika ya 90+7.

Kwa matokeo hayo Chelsea wamepanda mpaka nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza na kufikisha alama 60 katika michezo 37 waliyocheza na kuwafanya kuwa hatua moja mbele kushiriki michuano ya Europa Conference msimu wa 2024/25 na hatua nyingine kushiriki michuano ya Europa League kwa msimu ujao.

Kama Chelsea atapata ushindi katika mechi yake ya Mwisho dhidi ya Bournemouth basi atafikisha alama 63 sawa na Totenham Hotspurs wenye alama 63 na endapo Totenham watapoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Shiffield United basi Chelsea watashiriki michuano ya EUROPA LEAGUE .

Kama watakosa nafasi ya kushiriki Europa basi watalazimika kupata sare ama kushinda mchezo wao wa mwisho wa msimu dhidi ya ya Bournemouth ili kujihakikishia nafasi ya ushiriki wa michuano ya UEFA CONFERENCE. Kama Chelsea watapoteza mchezo huo wa mwisho na Newcastle akashinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Brentford basi Chelsea hawatashiriki michuano yoyote ya ulaya kwa msimu ujao.


Post a Comment

0 Comments