XABI ALONSO AWEKA REKODI MPYA BUNDESLIGA

 Hatimaye klabu ya Bayern Leverkusen imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kwanza wa Bundesliga kwa msimu wa 2023/24. Timu hiyo chini ya Xabi Alonso imetangazwa kuwa bingwa ikiwa imesalia michezo 7 ambayo haijachezwa. 

Leverkusen wametwaa ubingwa huo baada ya kucheza michezo 29 wakipata sare michezo 25 na kutoka sare michezo minne wakiwa hawajafungwa mchezo wowote na kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote. ndani ya Bundesliga timu hiyo imefanikiwa kufunga mabao 74 wakifungwa mabao 19 pekee

Bayern Leverkusen imekuwa na msimu mzuri mno baada ya kutopoteza  mechi 43 mfululizo katika michuano mbalimbali iliyoshiriki.

Mpaka sasa timu hiyo imebakiwa na makombe mawili mkononi ikiwemo fainali ya DFB POKAL dhidi ya FCK na mashindano ya Europa League ambayo wapo robo fainal dhidi ya Westaham.

Post a Comment

0 Comments