BETI NASI UTAJIRIKE

LIVERPOOL NA ARSENAL ZAKALIA KUTI KAVU MANCHESTER CITY IKIPETA KILELENI

 Mashabiki wa Arsenal na Liverpool wamejikuta wakimaliza wikiendi vibaya baada ya timu zao kupoteza michezo muhimu kuelekea ubingwa wa EPL msimu wa 2023/24.



Liverpool wakiwa nyumbani ANFIELD waliambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Crystal Palace bao lililofungwa na Eze dakika ya 14 ya mchezo akimalizia pasi iliyopigwa na Mitchel. kwa matokeo hayo Liverpool imeshuka mpaka nafasi ya tatu ikiwa na pointi 71 sawa na Arsenal baada ya kucheza michezo 32 ya Ligi kuu.

Arsenal wakiwa dimba la nyumbani EMIRATES waliambulia kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Aston Villa mabao yaliyofungwa na Bailey dakika ya 84 na Watkins dakika ya 87. Kwa matokeo haya Arsenal wamesalia nafasi ya pili wakiwa na alama 71 sawa na Liverpool na wote wamecheza michezo 32.

Mpaka sasa timu zote zimesalia michezo 6 kuweza kukamilisha msimu wa 2023/24 huku Manchester City wakiongoza msimamo wa ligi wakiwa na alama 72 baada ya kucheza michezo 32.hii hapa orodha ya michezo iliyobaki kwa vigogo hawa wa EPL

Manchester City amebakiwa na michezo sita muhimu na kama atashinda yote basi atajinyakulia ubingwa wa EPL kwa mara ya nne mfululizo na kuweka rekodi mpya ambayo haijawahi kuwekwa 

michezo ya Manchester city ni dhidi ya

1.Brighton 

2.Nottingham Forrest

3.Wolverhampton

4.Fulham 

5.Tottenham 

6.Westham 

michezo ya Arsenal dhidi ya 

1.Wolverhampton

2.Chelsea

3.Tottenham

4.Manchester United 

5.Bournemouth

6.Everton

Michezo ya Liverpool dhidi ya 

1.Fulham

2.Everton 

3.Westham

4.Aston villa

5.Tottenham

6.Wolverhampton



Post a Comment

0 Comments