Klabu ya Azam FC imeendelea kufanya vyema michezo yake ya ligi kuu ( NBC premier League) baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC.
Katika mchezo huo uliopigwa Majaliwa Stadium, Azam FC walipata mabao hayo mawili yaliyofungwa na Kipre Junior dakika ya 63 na 84. kwa matokeo hayo Azam amefikisha alama 50 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 22 na sasa anakuwa nafasi ya pili nyuma ya Yanga SC.
Kwa hesabu za haraka Azam FC ana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kama atashindwa kufanya hivyo basi akimaliza nafasi ya pili msimu ujao atashiriki ligi ya mabingwa Africa.
0 Comments