Mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris St-Germain Kylian Mbappe, 25, amesema kamwe hatojiunga na klabu ya Arsenal mwishoni mwa msimu kwa kuwa Uingereza kuna baridi kali. (Mail)
Winga Muingereza Cole Palmer, 21, anayecheza katika kblu ya Chelsea anatarajiwa kupokea nyongeza kubwa ya mshahara. Nyongeza hiyo inakuja ikiwa bado hata hajatimiza mwaka mmoja toka alipojiunga na klabu hiyo akitokea Manchester City. (Star)
Viongozi wa klabu ya Nice wanajiandaa kukwamisha jitihada za Manchester United kutaka kumsajili beki wao wa kati Mfaransa Jean-Clair Todibo, 24. (Football Insid
Klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani imeipatia Tottenham Hotspur muda wa mwisho wa kumnunua mshambuliaji Timo Werner, 28, ambaye walimsajili kwa mkopo toka mwezi Januari. (Express)
Manchester City wanataka kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na golikipa wao Ederson, 30. (Star)
Newcastle United na Chelsea wanajiandaa na mbio za kutaka kumsajili winga raia wa Ufaransa anayechezea klabu ya Lyon, Rayan Cherki, 20. (Fichajes - in Spanish)
Beki wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Korea Kusini Kim Min-jae, 27, hana furaha na maisha katika klabu hiyo ya Ujerumani. Kim alishawahi kuwindwa na Manchester United. (t-online, via Football Transfers)
Klabu ya Al-Ahli ya nchini Saudi Arabia imeweka wazi nia yao ya kumsajili kiungo wa Argentina Rodrigo de Paul, 29, kutoka klabu ya Atletico Madrid. (Fichajes - in Spanish)
Kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate amemuarifu mshambuliaji wa Manchester United, ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Getafe, Mason Greenwood, 22, kuwa hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki michuano ya Euro 2024. Hata hivyo Southgate hakuzungumzia uwezekano wa kurudisha kikosini baada ya michuano hiyo. (Express)
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy, 47, amekataa ofa mbalimbali za kufundisha vilabu sehemu tofauti barani Ulaya – sababu ikiwa ni nia ya Mholanzi huyo anataka kufundisha katika ligi ya England. (Mirror)
0 Comments